Featured Stories / News

WITO UMETOLEWA KWA WAHUDUMU WA AFYA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT KUFANYA MAZUNGUMZO NA SEREKALI YA KAUNTI ILI KUMALIZA MGOMO AMBAO UMEATHIRI SEKTA YA AFYA HAPA JIMBONI.

Na JB Nateleng,  Wito umetolewa kwa wahudumu wa afya katika kaunti ya Marsabit kufanya mazungumzo na serekali ya kaunti ili kumaliza mgomo ambao umeathiri sekta ya afya hapa jimboni. Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Chifu wa lokesheni ya Kalacha Sabdio Wario amesema kuwa itakuwa ni afueni iwapo[Read More…]

WAKAAZI WA MARSABIT WATOA HISIA ZAO KUHUSIANA NA UAMUZI WA MAHAKAMA ULIOPIGA MARUFUKU HAZINA YA MAENEO BUNGE NCHINI NG-CDF

Na Isaac Waihenya & Abdiaziz Abdi & Kame Wario, Wakaazi wa Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na uamuzi wa mahakama uliopiga marufuku hazina ya maeneo bunge nchini NG-CDF. Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani wametaja kugadhabishwa na hatua hiyo ya mahakama ambayo wameitaja kama inayohujumu haki zao. Wametaja[Read More…]

WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT KUDUMISHA USAFI ILI KUJIZUIA DHIDI YA MARADHI YANAYOTOKANA NA UCHAFU.

NA NAIMA MOHAMMED Wito umetolewa kwa wananchi katika kaunti ya Marsabit  kudumisha usafi ili kujizuia dhidi ya maradhi yanayotokana na uchafu. Kwa mujibu wa afisa anayesimamia maswala ya usafi katika kaunti ya Marsabit Chris Mabonga ni kuwa baadhi ya magonjwa ambayo yanaripotiwa hapa jimboni Marsabit yanaweza epukika iwapo wananchi watadumisha[Read More…]

SERIKALI ITAANZA KUFANYA VIKAO VYA KUSHIRIKISHA UMMA KUHUSU UMUHIMU WA VITAMBULISHO VYA KIDIJTALI, MAISHA CARD.

NA CAROLINE WAFORO Serikali itaanza kufanya vikao vya ushirikishwaji wa umma kuhusu umuhimu wa vitambulisho vya kidijtali, maisha card. Vikao hivyo vitakavyoanza mwezi huu wa Septemba vitaongozwa na machifu huku wakaazi jimboni Marsabit wakitakiwa kuhudhuria. Haya yamewekwa wazi na naibu kamishna wa Marsabit ya kati Kefa Marube wakati wa kikao[Read More…]

UTEPETEVU WA WAZAZI WATAJWA KAMA MOJAWEPO YA MASWALA YANAYOPEKEA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI JIMBONI MARSABIT.

Na JB Nateleng, Utepetevu wa wazazi katika kuwalea wanao umetajwa kama sababu inayochangia katika kuongezeka kwa maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI. Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Imam wa miskiti ya Jamia jimboni Marsabit Sheikh Mohamed Noor amesema kuwa, wazazi wengi wamelegeza majukumu yao ya kuwalea wanawao[Read More…]

WASHIKADAU KATIKA SEKTA YA ELIMU WATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUTAFUTA SULUHU LA KUDUMU KUHUSU VISA VYA MOTO SHULENI.

Na JB Nateleng, Washikadau wa elimu wanafaa kuketi chini na wazazi pamoja na wakuu wa shule zote ili kuhakikisha kuwa wametoa suluhu la kudumu kuhusiana na kero la shule kuchomwa. Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani ofisini mwake, mkurugenzi wa shirika la MWADO,Nuria Gollo ni kuwa wanafunzi wanachoma shule kusubuka[Read More…]

MAAFISA WA POLISI MJINI MARSABIT WAENDELEZA MSAKO WA POMBE HARAMU.

Na Caroline Waforo, Maafisa wa polisi pamoja kwa ushirikiano na machifu wanaendeleza msako wa pombe haramu pamoja na mihadarati mjini Marsabit. Operesheni hiyo iliyongo’a nanga alhamisi wiki jana inapania kuhakikisha kuwa utumizi wa pombe haramu pamoja na mihadarati unakomeshwa kikamilifu kulingana na kamanda wa polisi Leonard Kimaiyo. Aidha wamiliki wa vilabu[Read More…]

Subscribe to eNewsletter