Highlights

Maafisa wa usalama Laisamis waimarima msako kumkamata mshukiwa wa ulawiti Logologo.

NA Nyabande Orwa

Maafisa wa usalama katika kaunti ndogo ya Laisamis wanaendelea na msako mkali dhidi ya mshukiwa mwenye umri wa miaka 16 anayetuhumiwa kumlawiti mvulana wa miaka 10 siku ya Jumapili katika eneo la Logo Logo.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, OCPD wa Laisamis, Mohamed Mwakio, amesema kuwa kwa sasa wanashirikiana kwa karibu na wazee wa amani katika eneo hilo ili kumtambua mshukiwa na kufanikisha kukamatwa kwake.

Mwakio amesema tayari faili ya mshukiwa imeandaliwa, na pindi atakapokamatwa atachukuliwa alama za vidole na kufikishwa mahakamani mara moja.

Wakati huo huo, Mwakio ameongeza kuwa hali ya afya ya mwathiriwa imeimarika baada ya kutibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment