Highlights

Wito wa kukomesha ukeketaji wa wasichana laisamis watolewa

NA Samuel Kosgei

Mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka eneo bunge la Laisamis, kaunti ya Marsabit, Rose Orguba, amesema njia kuu ya kukomesha ukeketaji wa wasichana ni kuhakikisha wanapata elimu.

Akizungumza na kituo hiki pembezoni mwa hafla moja mjini Merile, Orguba alisema wasichana wengi wanaoendelea kufanyiwa ukeketaji ni wale ambao hawaendi shule. Alieleza kuwa wasichana wanaosoma mara nyingi hukataa kufanyiwa ukeketaji au hata kutoroka, tofauti na wale wasiopata fursa ya elimu.

Orguba hata hivyo amebainisha kuwa ingawa visa vya ukeketaji vinaendelea kupungua katika eneo hilo, dhulma hiyo bado huripotiwa hasa wakati wa likizo ndefu za shule.

Amewataka wazazi kuachana na mila hiyo, akisisitiza kuwa ukeketaji ni dhulma inayokiuka haki za mtoto wa kike.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment