Highlights

World Vision na Serikali ya Kaunti Kuimarisha Huduma za Maji North Horr

Na JB Nateleng

Shirika la World Vision Kenya kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Marsabit zimetia saini makubaliano ya kutekeleza miradi miwili ya maji katika eneo la North Horr, ikiwa ni juhudi za kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama.

Miradi hiyo inatarajiwa kuwanufaisha takriban watu 9,700 wanaokabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji katika eneo hilo.

Kupitia ushirikiano huo, Serikali ya Kaunti ya Marsabit kwa kushirikiana na Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge ya North Horr (NG-CDF) zitasimamia uchimbaji wa visima na kazi nyingine za kiufundi. Nayo World Vision Kenya itafadhili uwekaji wa mifumo ya nishati ya jua ya kusukuma maji, ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi na kusambaza maji, pamoja na kuwapa wanajamii mafunzo ya kusimamia na kutunza miradi hiyo.

Wadau hao wamesema ushirikiano huo utasaidia kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama, kuboresha afya ya wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika eneo la North Horr.

Post Comment