Highlights

Viongozi wa kisiasa nchini watakiwa kujiepusha na matamshi ya uchochezi

Na Caroline Waforo

Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Marsabit na kote nchini wametakiwa kujiepusha na matamshi ya uchochezi yanayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa kitaifa, huku nchi ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kupitia taarifa ya pamoja, Baraza la Viongozi wa Kidini (Interfaith Council) tawi la Marsabit, limedokeza kuwa matamshi yanayotolewa na baadhi ya viongozi nchini yanaweza kuchochea migawanyiko na kuhatarisha usalama wa taifa iwapo hayatazingatiwa kwa umakini.

Askofu wa Kanisa la Kianglikana katika kaunti ya Marsabit Daniel Qampicha, amewataka viongozi kuhubiri amani badala ya kutumia lugha inayoweza kuibua chuki miongoni mwa jamii.

Baraza hilo pia limeelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa magenge ya wahuni katika baadhi ya mikutano ya kisiasa na kuwataka vijana kutokubali kutumiwa na wanasiasa kuzua fujo nchini.

Aidha viongozi hao wamewahimiza wananchi wenye sifa kujitokeza kuendelea kujiandikisha kama wapiga kura.

Post Comment