Mwanaume apigwa faini ya shilingi 200,000 kwa kutishia kumuua babake, Marsabit Central
Na Mwandishi wetu
Mahakama ya Marsabit imempiga faini ya shilingi 200,000 au kifungo cha miaka 6 gerezani mwanaume mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kumtishia maisha babake mzazi.
Kwa mujibu wa mashtaka, Jattani Kanu Ali amepatikana na hatia ya kutishia kumuua babake Kanu Ali Qittoh siku ya hapo jana Jumatano katika eneo la Mata Arba, kaunti ndogo ya Marsabit Central.
Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo ya Marsabit Edward Oboge, baada ya mshtakiwa kukiri kosa dhidi yake.
Akiwasilisha ushahidi wake mahakamani, mwathiriwa alieleza kuwa maisha yake yamo hatarani kutokana na vitisho vya mwanawe. Pia alieleza mahakama kuwa mwanawe amekuwa akimtukana na kumdhalilisha mara kwa mara.
Mhukumiwa ana siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.



Post Comment