Highlights

Seneta Chute ataka maelezo kuhusu hati za ardhi Nyayo Road

Na Abdilaziz Yusuf

Seneta wa Kaunti ya Marsabit, Mohamed Said Chute, ameishinikiza Wizara ya Ardhi kueleza sababu za kucheleweshwa kwa utoaji wa hati miliki za ardhi kwa wanufaika wa viwanja 214 vilivyoko Nyayo Road mjini Marsabit.

Akizungumza katika Bunge la Seneti , Seneta Chute amesema wakazi walipewa barua za ugavi wa viwanja mwaka 2018 na kulipa ada zote zinazohitajika mwaka 2024, lakini hadi sasa hawajapokea hati miliki zao licha ya kukamilisha masharti yote yaliyowekwa na serikali.

Aidha ameitaka wizara kueleza hatua ambazo imechukua kuharakisha utoaji wa hati hizo na kutoa ratiba maalum ya lini wanufaika watapokea hati miliki zao.

Hata hivyo amesema ahadi za mara kwa mara bila tarehe ya utekelezaji haziwapi wananchi uhakika, akisisitiza kuwa wakazi wa Marsabit wamekuwa wakisubiri kwa zaidi ya miaka mitatu tangu walipokamilisha malipo.

1 comment

comments user
Chocolate Moulds

Founded in Istanbul in 1980, Implast is one of the world’s leading experts in chocolate mould manufacturing, guided by an unwavering commitment to quality. Using the highest-grade polycarbonate raw materials in our production processes, we deliver products that are fully compatible with all chocolate production lines. The moulds we produce with our premium raw material selection and flawless craftsmanship are true works of mastery that support your success in the industry.

Post Comment