Highlights

Mwanaume ashtakiwa kwa kumpiga busu mwanamke mmoja bila idhini yake mjini Marsabit

Mwanaume mmoja ameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa tuhuma za kutishia kuua.

Mshukiwa Galgallo Boru anadaiwa kumtishia maisha babake mnamo siku ya Jumapili ya tarehe 2 mwezi Agosti katika lokesheni ya Jirime kaunti ndogo ya Marsabit Central.

Mbele ya Hakimu Mkuu mwandamizi wa mahakama hiyo ya Marsabit Christine Wekesa leo Jumatano, mshukiwa amekanusha shtaka dhidi yake.

Mahakama imemwachilia mshukiwa kwa bondi ya shilingi 50,000 au pesa taslimu 20,000.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 17 mwezi huu wa Agosti.

wakati huo huo

Mwanaume mmoja ameshtakiwa katika mahakama hiyo ya Marsabit kwa tuhuma za kumpiga busu mwanamke mmoja bila idhini yake.

Mshukiwa Kiya Bonaya anadaiwa kutekeleza kosa hilo kwa makusudi siku ya Jumatatu, tarehe 3 mwezi Agosti, katika lokesheni ya Mountain kaunti ndogo ya Marsabit Central.

Mbele ya Hakimu Mkuu mwandamizi Christine Wekesa leo Jumatano, mshukiwa amekanusha kosa hilo.

Mahakama imemwachilia mshukiwa kwa bondi ya shilingi 50,000 au pesa taslimu 20,000.

Kesi hiyo imeratibiwa kusikilizwa tarehe 3 mwezi Septemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa sheria za Kenya, kitendo chochote cha kumgusa mtu kingono bila idhini yake kinaweza kujumuisha makosa ya kingono na hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, kulingana na mazingira ya tukio na mashtaka yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka.

Post Comment