Highlights

Vijiji 30 vya Marsabit Central Vyakabidhiwa Mahema ya Viti 50

Na JB Nateleng

Vijiji 30 katika wadi ya Marsabit Central, kaunti ya Marsabit, vimenufaika na mahema yenye uwezo wa kubeba watu 50 kila moja, yaliyotolewa na serikali ya kaunti ya Marsabit kupitia idara ya jinsia kwa ushirikiano na ofisi ya mwakilishi wadi wa Marsabit central kwa lengo la kusaidia katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Wakazi waliopokea mahema hayo wameeleza kuridhishwa na mpango huo, wakisema utawasaidia kuandaa shughuli mbalimbali za kijamii kama vile harusi, mikutano ya kijamii, mazishi na hafla nyingine bila kulazimika kukodisha mahema kutoka maeneo ya mbali.

CUE IN… WAKAZI ON HEMA.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa mahema hayo, waziri wa jinsia na utamaduni katika kaunti ya Marsabit, Armara Galwab amesema mpango huo ulipendekezwa na wananchi kupitia mchakato wa ushirikishwaji wa umma, ambapo walitaka serikali ya kaunti kuipa kipaumbele akisema kwama serikali imezingatia maoni ya wananchi na itaendelea kuwezesha vijiji zaidi ili kuhakikisha jamii inanufaika na mpango huo wa maendeleo.

CUE IN… GALWAB ON HEMA

Naye mwakilishi wadi ya Marsabit Central, Jack Elisha, amewataka wanufaika kuhakikisha mahema hayo yanatumika kwa manufaa ya jamii nzima badala ya kutumiwa kwa maslahi binafsi akielezea kuwa mali hiyo ni ya umma na inapaswa kusimamiwa kwa uwazi na uwajibikaji ili iweze kuwahudumia wakazi kwa muda mrefu na kuchangia maendeleo ya jamii katika Wadi ya Marsabit Central.

CUE IN… JACK ON HEMA

Post Comment