Highlights

Parokia ya Kalacha kuandaa warsha ya siku nne ya vijana.

Na JB Nateleng

Parokia ya Kristo Maddo Jirrena Kalacha katika Dayosisi ya Marsabit itaandaa warsha ya siku nne kwa vijana, kuanzia tarehe 5 hadi 8 Agosti 2026, kwa lengo la kuwaimarisha kiimani na kuwapatia ushauri nasaha.

Akizungumza na idhaa hii, Padri mlezi wa vijana wa Parokia ya Kalacha, John Lekamaya, amesema warsha hiyo itawakutanisha vijana hao ili kuwahamasisha, kuwajengea imani ya kikatoliki na kuwafundisha mafundisho ya Kanisa.

Padri Lekamaya amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila kijana kushiriki katika warsha hiyo, akisema itachangia kuimarisha malezi ya Kikristo, kukuza maisha ya kiroho na kuwasaidia vijana kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika jamii.

Post Comment