Highlights

Wawili wafariki katika ajali ya barabarani karibu na dampsite, Marsabit

Na Nyabande Orwa

Watu wawili wameaga dunia na wengine 4 kujeruhiwa kutokana na ajali ya barabarani iliyohusisha magari mawili kwenye barabara ya Marsabit kuelekea Segel, karibu na eneo la kutupa taka, kaunti ya Marsabit.

Akithibitisha mkasa huo uliotokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo Jumatatu, kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Marsabit central, Beethoven Gachago amesema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Hilux na Toyota land Cruiser.

Gari aina ya Toyota Hilux lilikuwa linasafiri kutoka mjini Marsabit kuelekea Segel , ili hali Toyota land Cruiser lilikuwa linatoka eneo la Segel kuelekea Marsabit.

Wakati wa ajali hiyo, gari la Toyota Land Cruiser lilikuwa limeegeswa likikarabatiwa baada ya kukumbana na hitilafu kwenye magurudumu yake.

Gachago amesema mtu mmoja alifariki papo hapo, huku mwingine akifariki akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Marsabit. Mkuu huyo wa polisi amewarai madereva kuwa waangalifu barabarani.

Post Comment