Highlights

Serikali ya kaunti ya Marsabit yatenga shilingi milioni 300 kukabiliana na atharai za mvua ya El Nino.

Na Nyabande Orwa

Kaimu katibu wa kaunti ya Marsabit, Joseph Guyo, amesema serikali ya kaunti imetenga shilingi milioni300 kwa ajili ya maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha kati ya miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba, kulingana na utabiri wa Idara ya hali ya hewa nchini.

Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali za kaunti, Guyo amesema sehemu kubwa ya fedha hizo imeelekezwa katika sekta ya afya ili kuhakikisha hospitali ziko tayari kuhudumia wananchi endapo kutatokea majeruhi au magonjwa yatakayosababishwa na mafuriko na majanga mengine yanayoweza kuletwa na mvua hizo.

Cue In: Joseph Guyo on El Niño Plan

Wakati huo huo, waziri wa Mazingira wa kaunti ya Marsabit, Janet E. Ahatho, amesema serikali ya kaunti imeweka mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema kuendelea kuongezeka kwa kina cha maji katika Ziwa Turkana kumeathiri makazi na maisha ya wananchi wanaoishi maeneo ya ufuo, hivyo serikali inaendelea kutafuta suluhu za muda mfupi na za kudumu.

Cue In: Janet E. Ahatho

Post Comment