Highlights

Polisi waendeleza oparesheni kufuatia wizi wa ngamia Hawaye

Na Nyabande Orwa

Maafisa wa usalama katika kaunti ndogo ya Marsabit ya kati wanaendelea na oparesheni ya kuwasaka wahalifu wanaodaiwa kuiba ngamia 30 katika eneo la Hawaye, eneo bunge la North Horr, kaunti ya Marsabit.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Marsabit, Leonard Kimaiyo, amethibitisha tukio hilo akisema ngamia hao waliibwa jana jioni. Hata hivyo, amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa uhalifu huo.

Kimaiyo amesema oparesheni hiyo inahusisha vikosi mbalimbali vya usalama ambavyo vinaendelea na msako mkali ili kuwakamata wahusika na kurejesha mifugo iliyoibwa.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na maafisa wa usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini na kuwakamata wahuni hao ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Post Comment