Highlights

Bunge la kaunti ya Marsabit latenga shilingi Milioni 60 kuwalipa CHPS

NA Nyabande Orwa

Bunge la Kaunti ya Marsabit limetenga shilingi milioni 60 katika bajeti ya ziada ya mwaka wa kifedha 2025/2026 ili kulipa malimbikizi ya mishahara ya maafisa wa afya wa nyanjani, maarufu kama CHPs.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya bajeti, Daud Tomasot, wawakilishi wa wadi wanaendelea kufuatilia kwa karibu serikali ya kaunti ili kujua malipo hayo yamefikia wapi. Amesema haieleweki kwa nini maafisa hao hawajalipwa hadi sasa, ilhali fedha za kuwalipa zilipitishwa na bunge la kaunti.

Tomasot ametoa wito kwa kila mwakilishi wadi kufuatilia hali ya maafisa wa afya katika maeneo yao, ili kubaini ni miezi mingapi wanadai mishahara.

Kwa upande wake, mwanachama wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwakilishi wa wadi ya Loiyangalani, Daniel Emojo, amesema malalamiko ya maafisa hao ni ya kweli na yamewafikia. Amehoji kwa nini bado hawajalipwa na serikali ya kaunti ya Marsabit, ilhali serikali kuu inatekeleza wajibu wake wa kuwalipa kila mwezi.

Katika kikao cha leo cha ushirikishwaji wa umma kuhusu bajeti hiyo ya ziada ya zaidi ya shilingi bilioni 11, wawakilishi wadi wamewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kuchagua miradi itakayowanufaisha.

Jack Elish, Mwakilishi wa wadi ya Marsabit Central, amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika mchakato huo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment