Lori la ngano lapinduka eneo la KBC Marsabit, watu wawili wakiponea na majeraha madogo.
Na Nyabande Orwa
Watu wawili wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa likisafirisha ngano kupinduka katika eneo la KBC, mjini Marsabit, adhuhuri ya leo.
Kwa mujibu wa polisi wa Marsabit, dereva wa lori hilo alisema kuwa gari lilipoteza mwelekeo kabla ya kupinduka kando ya barabara. Waliojeruhiwa ni dereva na utingo, ambao walipata majeraha madogo na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Marsabit.
Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo. Tukio hili linajiri siku chache baada ya ajali nyingine kutokea katika eneo la Hula Hula kwenye barabara ya Marsabit–Moyale, ambapo mtu mmoja alipoteza maisha huku mwenzake akijeruhiwa.



Post Comment