Highlights

Wakazi wa Badassa,  Dirib Gombo walalamikia ubovu wa barabara.

Na JB Nateleng

Biashara na shughuli za usafiri zimetatizika leo kwenye barabara ya Marsabit–Badassa–Dirib Gombo baada ya wakazi kuandamana kulalamikia ubovu wa barabara hiyo.

Wakizungumza na wanahabari, wakazi hao wameilaumu mamlaka ya ujenzi wa barabara kuu (KeNHA) kwa kile walichodai ni kuchelewesha ukarabati wa barabara hiyo.

Wakazi hao wanasema hali hiyo imeathiri usafiri, biashara,usalama na upatikanaji wa huduma muhimu katika maeneo hayo.

Pia wanasema barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa inaunganisha kaunti za Marsabit, Wajir na Isiolo, huku wakitoa wito kwa viongozi wa kaunti ya Marsabit kusaidia katika kuwasilisha malalamishi yao kwa KeNHA ili ukarabati uanze haraka.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment