Highlights

Naomi Waqo akanusha kujiondoa mbio za ugavana Marsabit 2027.

Na Samuel Kosgei

Mwakilishi wa Wanawake katika Kaunti ya Marsabit, Naomi Jillo Waqo, amepuuzilia mbali uvumi unaodai kuwa amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha ugavana wa Marsabit mwaka 2027.

Akizungumza na meza ya Shajara, Naomi amesema kuwa hawezi kujiondoa kwa vyovyote vile, akisisitiza kuwa ni haki yake ya kikatiba kuwania kiti chochote anachotamani kama kiongozi.

Aidha, amepigia debe uongozi wa wanawake akisema kuwa wana uwezo wa kuongoza vyema bila kujihusisha na ubadhirifu wa mali ya umma. Amewarai wote watakaowania kiti cha ugavana kuheshimu kila mgombea na kuepuka propaganda pamoja na siasa duni.

Wakati huo huo, amewataka vijana kuongeza juhudi katika majukumu yao, hasa masomoni, ili kuepuka kujiingiza katika uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya. Pia ameiomba jamii kudumisha tamaduni nzuri na kuachana na zile potovu, ikiwemo mimba za mapema na ukeketaji.

Vilevile, amewapongeza wakaazi wa Kaunti ya Marsabit kwa kudumisha amani na usalama katika kipindi chote cha Ramadhan, huku akiwatakia Waislamu wote sherehe njema za Idd.

Post Comment