Highlights

Walengwa wa HSNP Marsabit watakiwa kusubiri malipo ya mwezi mmoja

Na Nyabande Orwa

Siku chache baada ya walengwa wa mpango wa Hunger Safety Net Programme (HSNP) katika kaunti ya Marsabit kupokea malipo ya miezi minne kutoka kwa serikali kuu, usimamizi wa mpango huo umewataka walengwa kuwa na subira kuhusu malipo ya mwezi uliosalia huku mipango ikiendelea kuhakikisha fedha hizo zinafika kwao.

Akizungumza na kituo hiki, meneja wa HSNP katika Kaunti ya Marsabit, Jonah Samana, amesema tayari maandalizi na taratibu muhimu zimekamilishwa, na walengwa watapokea malipo ya mwezi huo wakati wowote punde yatakapokuwa yameidhinishwa.

Kauli hiyo inajiri siku chache baada ya baadhi ya walengwa kulalamikia kutopokea malipo ya miezi mitano kama ilivyokuwa imetarajiwa, badala yake wakapokea fedha za miezi minne pekee.

Post Comment