Highlights

Uchunguzi waendelea kufuatia tukio la mtu kudungwa kisu Majengo

Na Mwandishi wetu

Polisi mjini Marsabit wanaendeleza uchunguzi kuhusu tukio la mtu mmoja kudungwa kisu katika eneo la Majengo, lililotokea siku ya Jumamosi.

Akizungumza na kituo hiki, mkuu wa idara ya upelelezi (DCI) katika kaunti ya Marsabit, Kennedy Nyaga, amesema mshukiwa, Yusuf Wario, aliachiliwa kwa bondi ya polisi huku uchunguzi ukiendelea.

Nyaga amesema mwathiriwa, Alkano Huka, alipatiwa matibabu katika hospitali ya Avanah na baadaye kuruhusiwa kwenda nyumbani. Hata hivyo, alitafuta matibabu zaidi katika Hospitali ya rufaa na mafunzo ya Marsabit, ambapo alielekezwa kuendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Meru.

Kwa mujibu wa Nyaga, uchunguzi wa awali unaonyesha wawili hao walikuwa na tofauti zao za kibinafsi, ingawa chanzo halisi cha mzozo huo bado hakijabainika.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment