Mtu mmoja auawa, na mwingine akijeruhiwa katika shambulizi la Dabel.
Na Joyce Akinyi
Mtu mmoja ameuawa huku mwingine akijeruhiwa vibaya kufuatia shambulizi la kutumia bunduki lililotokea katika eneo la Dabel, kaunti ndogo ya Moyale, kaunti ya Marsabit.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa kaunti ya Marsabit, Leonard Kimaiyo, wahuni hao walitoroka na kifaa cha kutambua dhahabu mara tu baada ya kutekeleza shambulizi hilo.
Katika kisa hicho, Abdi Aziz Noor ambaye alikuwa akiliendesha pikipiki hiyo alijeruhiwa kwa risasi tumboni, huku abiria wake, Dayo Adan Abdullahi, mwenye umri wa miaka 21 akiaga dunia papo hapo.
Noor anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Moyale huku mwili wa mwenzake ukihifadhiwa katika makafani ya hospitali iyo hiyo. Kamanda Kimaiyo amesema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha shambulizi hilo kando na kuwasaka wahuni.



Post Comment