Highlights

Mwanaume ahukumiwa miaka miwili jela kwa kujaribu kutoroka mikononi mwa maafisa wa magereza, Marsabit

Mwanaume mmoja aliyejaribu kutoroka mikononi mwa maafisa wa magereza katika mazingira ya mahakama ya Marsabit majuma mawili yaliyopita, amehukumiwa kifungo cha miaka 2 gerezani au kutoa faini ya shilingi 100,000.

Joseph Wako mwenye umri wa miaka 20 alihukumiwa hapo jana Jumatatu na hakimu    Mkuu Mkaazi wa mahakama hiyo Christine Wekesa baada yake kukiri kosa dhidi yake.

Mahakama iliarifiwa kuwa tarehe 2 mwezi Machi maafisa wa magereza walikabiliana na mhukumiwa huyo na kumzuia kutoroka.

Hata hivyo, bado anakabiliwa na shtaka jingine la kutishia kuua, ambalo linaendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

1 comment

comments user
tripscan

This is the kind of media Africa needs — authentic, bold, and community-driven. Big up sana!

Post Comment