Highlights

Usalama waimarishwa Marsabit Central msimu huu wa mfungo wa Kwaresma na Ramadhani

NA Caroline Waforo

Idara ya usalama katika kaunti ndogo ya Marsabit Central imewahakikishia wakaazi usalama wa kutosha msimu huu wa mfungo wa Kwaresma pamoja na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza na Shajara OCPD wa Marsabit Central Beethoven Gachago, amesema kuwa maafisa wa polisi wameimarisha doria ili kuhakikisha kuwa waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu wanatekeleza ibada zao kwa amani na utulivu.

Aidha amewahimiza wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa mapema kuhusu mienendo yoyote ya kutiliwa shaka ili kuzuia visa vya uhalifu.

Nao viongozi wa kidini wametakiwa kuendelea kuhubiri amani, mshikamano na uvumilivu miongoni mwa waumini.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment