Highlights

Mafuriko yawaacha familia 53 bila makazi Dumasho, Marsabit.

Na JB Nateleng

Takriban familia 53 zimeathirika kutokana na mvua huku nyumba nyingi ambazo ni za muda zikisombwa na maji katika Kijiji cha Dumasho kilichopo katika eneo la Dokatu, wadi ya Sagante Jaldessa, eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit.

Wakazi hao kwa sasa wanakabiliwa na hali ngumu baada ya kupoteza makazi yao, hali inayowaacha bila hifadhi salama.

Wakaazi hao wametoa wito kwa mashirika ya misaada kama vile Kenya Red Cross, serikali ya kaunti ya Marsabit pamoja na serikali kuu kuingilia kati na kuwasaidia.

Pia wamewasihi wadau wengine na wasamaria wema kujitokeza kutoa msaada wa dharura wa chakula, maji safi na makazi ya muda.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment