Highlights

IEBC yalenga kusajili wapiga kura wapya 40,000 Marsabit huku zoezi la usajili endelevu wa wapigaji kura likianza rasmi

Na Caroline Waforo

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imeanza rasmi zoezi la kitaifa la usajili endelevu wa wapigaji kura kote nchini, zoezi litakaloendelea kwa muda wa mwezi mmoja.

Katika kaunti ya Marsabit tume hiyo inalenga kusajili wapiga kura wapya 40,000 ikiwa ni juhudi za kuongeza idadi ya wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Akizungumza na Shajara afisini mwake, Msimamizi wa IEBC tawi la Marsabit Sanchan Lokadio amedokeza kuwa zoezi hilo linafanyika katika maeneo yote jimboni huku maafisa wa IEBC wakifika katika kila wadi ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata fursa ya kujisajili.

Kwa sasa kaunti ya Marsabit ina wapiga kura 166,000 huku tume hiyo ikilenga kufikisha idadi hiyo hadi 200,000 ifikapo uchaguzi mkuu ujao.

Aidha, Sanchan ametoa wito kwa wananchi haswa vijana wa kizazi cha GEN Z, kujitokeza kwa wingi na kujisajili kama wapiga kura.

Katika ngazi ya kitaifa tume ya IEBC inalenga kusajili wapiga kura wapya 2.5 milioni.

1 comment

comments user
Randell

From news to culture, you guys are preserving our identity. Respect kubwa sana to the entire team!

Post Comment