Viongozi kutoka eneo la Laisamis wamewataka wakaazi kuwa na subira huku serikali ikiendelea na operesheni ya kufuatilia na kurejesha mifugo iliyoibwa eneo la Gudas.
Na Sabalua Moses
Viongozi kutoka eneo la Laisamis wamewataka wakaazi kuwa na subira huku serikali ikiendelea na operesheni ya kufuatilia na kurejesha mifugo iliyoibwa eneo la Gudas.
Wakiongozwa na Mbunge wa Laisamis, Joseph Lekuton, viongozi hao wamepongeza serikali pamoja na vyombo vya usalama kwa juhudi zinazoendelea za kuhakikisha mifugo hiyo inapatikana na kurejeshwa kwa wamiliki wake.
Akizungumza na Shajara ya Redio Jangwani, Lekuton amewataka wanasiasa kuepuka kuingilia operesheni hiyo, akisema ni muhimu kuipa serikali na maafisa wa usalama nafasi ya kukamilisha kazi yao kwa utulivu.
Aidha, Lekuton amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani na ushirikiano kati ya wananchi na wadau mbalimbali ili kufanikisha juhudi za kurejesha mifugo hiyo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wadi ya Loglogo, Bernard Leakono, amesema serikali ina rasiliali za kutosha kuendeleza mchakato huo na kutaka wakaazi kudumisha amani.



Post Comment