Mama aliyejifungua watoto watano Marsabit aendelea kuimarika kiafya na watoto wake.
Na JB Nateleng
Mama aliyejifungua watoto watano katika Hospitali ya Rufaa ya Marsabit anaendelea kuimarika pamoja na watoto wake, huku madaktari na wauguzi wakiendelea kufuatilia hali yao ya afya.
Akizungumza na wanahabari, Muuguzi Mkuu wa Wodi ya Uzazi, Eleansy Karegi, amesema Nchauni Lemoitanit aliletwa hospitalini jana saa sita mchana na kujifungua watoto hao saa saba mchana bila matatizo yoyote.
Karegi amesema wahudumu wa afya wanaendelea kuwapa mama huyo na watoto wake huduma na uangalizi maalum, akibainisha kuwa wote wanaendelea vizuri chini ya usimamizi wa madaktari.
Aidha, amesema tukio hilo ni la kwanza katika historia ya Hospitali ya Rufaa ya Marsabit kwa mama kujifungua watoto watano kwa wakati mmoja.



Post Comment