Wazazi wahimizwa kuwahusisha watoto katika mafunzo ya dini wakati wa likizo
Na JB Nateleng
Huku wanafunzi wakitarajiwa kufunga shule na kurejea nyumbani kwa likizo ya mwezi Aprili, wazazi wamehimizwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki katika shughuli za Parokia ili kujifunza maadili ya dini ya Kikatoliki.
Wito huo umetolewa na Mtawa Mourine Awino Kutoka shirika la Assumption sisters of Eldoret anayehudumu kwa Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Moyale, katika Jimbo Katoliki la Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii, Mtawa Mourine amesema ni muhimu kwa watoto kuhusishwa kikamilifu katika masuala ya imani wakiwa wadogo, ili kuwajenga kiroho na kuwalea katika maisha ya kumcha Mungu, huduma na matendo mema ya kitume.
Aidha, amesisitiza kuwa watoto wa PMC wana ratiba maalum ya shughuli za kidini likizo hii, na ni jukumu la wazazi kuhakikisha watoto wao wanaifuata kwa manufaa yao pamoja na familia kwa ujumla.



Post Comment