Highlights

Seneta Chute aishinikiza kaunti kukamilisha kituo cha afya cha Uran

Na Abdilaziz Yusuf

Seneta wa Marsabit, Mohamed Said Chute, ameishinikiza serikali ya kaunti ya Marsabit kueleza hatua zinazochukuliwa kuhakikisha ujenzi wa kituo cha afya cha Uran unakamilishwa, pamoja na kukiwezesha kwa vifaa vinavyohitajika ili kianze kutoa huduma kwa wananchi ndani ya muda unaofaa.

Akizungumza katika kikao cha Seneti siku ya Jumatano, Seneta Chute ameitaka serikali ya kaunti kuwawajibisha wakandarasi au maafisa wa umma watakaobainika kusababisha kucheleweshwa kwa mradi huo.

Aidha, ameitaka kamati ya kudumu ya Seneti kuhusu afya kuwasilisha taarifa kuhusu hali ya sasa ya mradi huo, ikiwemo hatua iliyofikiwa katika ujenzi wake, pamoja na kufanyika kwa ukaguzi wa fedha zote zilizotengwa na kutumika katika utekelezaji wa mradi huo.

Post Comment