Highlights

Ukosefu wa sera wazorotesha ukusanyaji wa takwimu za mtoto wa kike Marsabit

Na Nyabande Orwa

Kama njia moja ya kuhakikisha kunakuwa na takwimu za kutosha kuhusu mtoto wa kike katika kaunti ya Marsabit ni viongozi kuweka sera nzuri. Haya yamesemwa na mwanaharakati na mwanasiasa wa Marsabit, Rose Orguba.

Akizungumza na kituo hiki mapema leo katika kipindi cha Amkia Jangwani, Orguba amewakosoa viongozi kwa kushindwa kuweka sera zitakazosaidia kukusanya takwimu muhimu.

Amesema takwimu hizo zitasaidia kuhakikisha mtoto wa kike anashirikishwa katika uongozi wa kaunti, na changamoto zake za elimu na afya zinatatuliwa.

Pia ameisihi serikali kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia katika ukusanyaji wa takwimu hizo.

Wakati huo huo, Orguba amesema teknolojia inaweza kusaidia kukusanya takwimu kwa urahisi, lakini viongozi lazima wajitume kuhakikisha inatumika vizuri, isiwe sababu ya uzembe.

Post Comment