Highlights

Kaunti ya Marsabit yatumia milioni 89.55 kwenye safari za ndani na nje katika nusu ya kwanza ya mwaka wa kifedha 2025-2026

Kaunti ya Marsabit imetumia shilingi milioni 73.65 katika safari za ndani katika nusu ya kwanza ya mwaka wa kifedha 2025-2026.

Kulingana na ripoti ya Mthibiti wa bajeti Margaret Nyakang’ bunge la kaunti ya Marsabit limetumia mgao mkubwa wa fedha hizo ambao ni shilingi milioni 55.04 huku serikali ya kaunti ikitumia shilingi milioni 18.62.

Ka upande wa safari za nje, jumla ya shilingi milioni 12.9 zimetumika ambapo bunge la kaunti limetumia 11.01 huku serikali ya kaunti ikitumia shilingi milioni 1.96

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa nyingi za safari zimefanyika nchini jirani ya Ethiopia ambapo mamilioni ya pesa yametumika.

Kwa mfano, kati ya tarehe 8 hadi 12 mwezi Desemba mwaka 2025 maafisa 7 wa bunge la kaunti walisafiri nchini Ethiopia kuhudhuria mikutano ya maendeleo kuhusu sekta mbalimbali kama vile nishati, kilimo, utalii na kilimo safari iliyogharimu milioni 3.1.

Gharama sawia ilikadiriwa kati ya tarehe 15 hadi 19 mwezi disemba mwaka 2025.

Aidha, kati ya tarehe 1 hadi 5 Desemba na 19 hadi 24 Desemba, safari nyingine 2 nchini Ethiopia ziligharimu shilingi milioni 2.7 kwa maafisa 7 wa bunge.

Mbali na Ethiopia, safari za nje pia zimefanyika katika mataifa ya Marekani, Ufaransa, Uhispania na Dubai.

Ripoti hii inafichua jinsi safari za ndani na nje zinavyochangia matumizi makubwa ya fedha za umma.

Post Comment