Highlights

Tahadhari ya magonjwa yatolewa msimu huu wa mvua

Na Caroline Waforo

Huku mvua zikiendelea kushuhudiwa katika kaunti ya Marsabit wakaazi wamehimizwa kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa yanayohusishwa na msimu huu.

Akizungumza na Shajara, Naibu Mkrugenzi wa Afya ya Umma katika kaunti ya Marsabit Sora Jattani, amesema kuwa magonjwa kama kipindupindu na malaria yako katika hatari ya kuzuka kutokana na mvua zinazoendelea kushuhudiwa.

Amesisitiza kuwa kudumisha usafi wa mazingira ya nyumbani na maeneo ya umma ni hatua muhimu katika kuzuia milipuko ya magonjwa hayo.

Jattani amewahimiza wakaazi kulala ndani ya neti zilizotiwa dawa ili kujikinga dhidi ya mbu wanaosababisha malaria.

Pia amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa maji hayasimami katika sehemu moja, ili kuzuia mazalia ya mbu.

Wakati huo huo amewashauri wakaazi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhamia katika meneo ya juu na salama ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment