Highlights

Naibu chifu wa Nyayo Road kata ya Nagayo ashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya matusi hadharani

Na Mwandishi wetu

Naibu Chifu wa Nyayo Road kata ya Nagayo Fatuma Nane Shege ameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kutumia lugha ya matusi katika sehemu ya umma kinyume na sheria.

Mahakama imelezwa kuwa mnamo tarehe 29 mwezi Januari mwaka 2026, katika mazingira ya mahakama ya Marsabit mshukiwa alitamka matamshi ya matusi kwa nia ya kuvuruga amani.

Mbele ya hakimu mkuu mkaazi wa mahakama hiyo ya Marsabit Christine Wekesa, mshukiwa amekana shtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi 50,000 au pesa taslimu shilingi 20,000.

Aidha hakimu Wekesa amewashauri mlalamishi na mshtakiwa kusuluhisha kesi hiyo kwa kutumia njia mbadala AJS.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 30 mwezi huu wa Machi.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment