Jumbe za amani na umoja zatolewa kuelekea Sherehe za Idd-Ul-Fitr.
Na JB Nateleng
Huku waumini wa dini ya Kiislamu wakitarajiwa kusherehekea sikukuu ya Idd-Ul-Fitr hapo kesho Ijumaa, jumbe za heri njema zimeendelea kutolewa, huku wakihimizwa kusherehekea kwa nia njema, amani na furaha.
Ujumbe wa hivi punde umetolewa na Mkurugenzi wa Elimu wa Jimbo Katoliki la Marsabit, Padri Abraham Ali, ambaye amewatakia waumini hao heri njema ya sikukuu ya Eid.
Akizungumza na Shajara Padri Abraham amesema kuwa mfungo mtakatifu wa Ramadhani ambao ulianza wakati mmoja na mfungo wa Kwaresma kwa Wakristo ni muhimu kwani waumini wa dini zote mbili hupata fursa ya kujitolea katika maombi, wakiliombea taifa, viongozi pamoja na wale wasiojiweza katika jamii.
Katika ujumbe wake, Padri Abraham amesisitiza kuwa maombi yanapaswa kuendelea hata baada ya kumalizika kwa miezi hiyo mitukufu, akiwahimiza waumini kuyafanya kuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa kuiombea nchi, watu na kudumisha amani.
Aidha, Padri Abraham amewarai waumini kuendeleza umoja na mshikamano wanaposherehekea sikukuu ya Eid.



Post Comment