Sheikh aonya dhidi ya pombe na mihadarati wakati wa Eid
Na JB Nateleng
Wito umetolewa kwa vijana kuwa makini wanapojiandaa kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr kesho.
Akizungumza na kituo hiki, Sheikh Mohamed Noor wa msikiti wa Jamia mjini Marsabit amesema baadhi ya vijana hujihusisha na vitendo visivyofaa wakati wa sherehe, na akawataka kujiepusha na tabia hizo.
Amesema kuna vijana wanaokunywa pombe na kutumia mihadarati kupita kiasi, jambo ambalo si zuri na linapaswa kukomeshwa.
Sheikh Noor ameonya kuwa sherehe ya siku moja isiwapelekee vijana kujidhuru kwa kile wanachokiita kusherehekea.
Aidha, amesema maandalizi ya Eid yamepangwa vizuri na kuwataka waumini kufuata ratiba zilizowekwa na misikiti yao.
Pia amewahimiza wanajamii kusaidiana na kuwajali wasiojiweza, akisema hiyo ndiyo maana halisi ya Eid al-Fitr.



Post Comment