Mvutano wa kisiasa kati ya rais Ruto na Gachagua wazua Hisia Marsabit
Na Nyabande Orwa
Huku siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 zikizidi kushika kasi nchini, wakazi wa kaunti ya Marsabit wametoa maoni tofauti kuhusu mvutano uliopo kati ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua na Rais William Ruto.
Wakizungumza na kituo hiki, baadhi ya wakazi wamekosoa malumbano kati ya viongozi hao wawili wakisema kuwa yanaipa nchi taswira mbaya. Wamesema si vyema kwa viongozi wakuu kurushiana maneno makali hadharani.
Kwa upande mwingine, baadhi ya wananchi wameunga mkono hatua ya Rais kujibu matamshi ya Gachagua, wakisema kuwa kama kiongozi wa taifa, ana haki ya kujitetea. Pia wameeleza kuwa baadhi ya wanasiasa wanatumia vibaya uhuru wa kujieleza uliopo kikatiba.
Wameonya kuwa siasa za matusi zinaweza kuleta mgawanyiko na hata kuhatarisha amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Hata hivyo, kuna wale wanaotaka washikadau kuingilia kati ili kusaidia kupunguza mvutano huo na kurejesha utulivu wa kisiasa nchini.



Post Comment