Highlights

Mfugaji mmoja auawa kwa kupigwa risasi Hawaye, Marsabit

Na Caroline Waforo

Mfugaji mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Hawaye lokesheni ya Shurr eneobunge la North Horr kaunti ya Marsabit.

Akithibitisha kisa hicho cha mchana wa leo Jumatano, Naibu Kamanda wa polisi katika kaunti ya Marsabit George Kipkoros amesema kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 20 alipigwa risasi wakati wa jaribio la wizi wa mifugo alipokuwa malishoni.

Kipkoros amesema kuwa hakuna mifugo iliyoibwa kufuatia hatua za haraka za wanakijiji waliotibua jaribio hilo la wizi wa mifugo.

Kulingana na Kipkoros uchunguzi wa kisa hicho umeanzishwa huku wananchi wakihimizwa kudumisha amani na kushirikiana na maafisa wa usalama.

Aidha, ametoa onyo kali kwa wahalifu wa wizi wa mifugo akisema kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua kali za sheria.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment