Highlights

Vijana Marsabit wahimizwa kusambaza semi za amani mitandaoni na kuasi semi za chuki

Na Sabalua Moses

Viongozi wa kidini katika kaunti ya Marsabit wamewataka vijana kuepuka kutumiwa vibaya na wanasiasa kusambaza semi za chuki na kauli zinazoweza kuvuruga amani katika jamii.

Akizungumza na Shajara Askofu wa kanisa la ACK Marsabit Qampicha Wario amesema ni jukumu la kila mmoja kuwa makini anapotumia mitandao ya kijamii, akisisitiza kuwa vijana wanapaswa kutumia majukwaa hayo kueneza jumbe za amani, mshikamano na uwajibikaji katika jamii.

Aidha, amesema kuwa ni haki ya wanasiasa kuwania viti mbalimbali vya uongozi, lakini akawahimiza kufanya kampeni zao kwa njia ya amani huku wakihimiza umoja miongoni mwa wakazi wa kaunti ya Marsabit.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Nyeri, Anthony Muheria, amewahimiza vijana kutafuta majukwaa sahihi ya kujieleza na kushiriki katika mazungumzo yenye kujenga jamii.

Hata hivyo, Muheria amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu ili kuepuka kupoteza muda mwingi katika majukwaa hayo.

Post Comment