Wito watolewa kwa vikundi maalum kujiandikisha kama wapigakura Marsabit
Na Sabalua Moses
Huku zoezi la usajili wa wapigakura likiendelea katika Kaunti ya Marsabit, watu wanaoishi na ulemavu wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Akizungumza na kituo hiki, mwenyekiti wa kikundi cha walemavu cha Saku Disabled Group katika eneo la Saku, John Galgalo Boru, amesema ni muhimu kwa watu wanaoishi na ulemavu kushiriki kikamilifu katika mchakato huo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Aidha, Boru ameihimiza Tume ya IEBC kuhakikisha kuwa vyama vya kisiasa vinawateua watu wenye ulemavu wakati wa uteuzi wa wawakilishi maalum katika mabunge ya kaunti na ya kitaifa.
Wadau ikiwemo watetezi wanasisitiza umuhimu wa ushiriki jumuishi katika masuala ya kidemokrasia, wakieleza kuwa kila kundi lina nafasi ya kuchangia uongozi wa nchi kupitia kura.



Post Comment