Featured Stories / News

ASILIMIA 74.2 YA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT HUNYONYESHA WATOTO CHINI YA SAA MOJA.

Na Grace Gumato Janga la ukame limetajwa kama mojawapo ya changamoto ambayo inachangia kina mama kutonyonyesha watoto wao  katika kaunti ya Marsabit. Akizungumza na idhaa hii  afisini mwake David Buke  Halakhe afisa naye simamia lishe katika kaunti ya Marsabit amesema uwepo wa ukame umechangia akina mama wengi kukosa lishe bora[Read More…]

MSAKO WA NYAVU HARAMU MOITE, LOIYANGALANI WAENDELEA.

Na JB Nateleng Kama njia moja wepo ya kutunza na kuhifadhi mazingira ya ziwa Turkana, viongozi wa Kitengo cha Usimamizi wa Ufuo (BMU) ya Moite Eneo wadi ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit wameanzisha zoezi la kusaka nyavu ambazo zilikuwa zimeharamishwa kutumika katika ziwa hiyo.. Kulingana na Andrew Dokoya ambaye ni[Read More…]

VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WAZIDI KUKASHIFU ONGEZEKO LA MAPENZI YA JINSIA MOJA NCHINI.

Na Lelo Wako Viongozi wa kidini mjini Marsabit wamekashifu kuenea kwa  uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja na visa vya ukahaba haswa miongoni mwa vijana. Msimamizi wa kanisa la katoliki parokia ya cathedral, Padri Tito Makhoha amekashifu uhusiano aina hiyo huku akiwaomba vijana wasishinikizwe katika kushiriki uhusiano wa jinsia moja.[Read More…]

NTERNS’ WA MARSABIT WAENDELEA KUSHINIKIZA SERIKALI YA KAUNTI KUWALIPA MARUPURUPU YA ZAIDI YA MIEZI SITA.

 Na Samuel Kosgei Vijana wanagenzi walioajiriwa na serikali ya kaunti kwa kandarasi ya mwaka mmoja wameendelea kutoa lalama zao ya kutolipwa marupurupu ya zaidi ya miezi sita. Wanagenzi hao ambao leo wamefanya kikao na kamati ya bunge la Marsabit kuhusu utawala wamerai wawakilishi wadi wao kuwasaidia kusukuma serikali kuwapa malipo[Read More…]

WATOTO 10 WALIODAIWA KUTEKWA NYARA MWANZONI MWA MWAKA HUU NA MHUBIRI MOJA KATIKA ENEO LA PARKISHON KAUNTI YA MARSABIT WAREJESHWA KWA FAMILIA ZAO.

Na Carol Waforo, Watoto 10 waliodaiwa kutekwa nyara mwanzoni mwa mwaka huu na mhubiri moja katika eneo la Parkishon kaunti ya Marsabit wamerejeshwa kwa familia zao. Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu afisa wa watoto hapa katika eneo bunge la Saku Medina Doko amesema kuwa watoto[Read More…]

WAKAAZI WA MARSABIT WATOA HISIA ZAO KUHUSIANA NA MAADAMANO YA VIJANA WA GEN ZS (NANENANE)

Na Ebinet Apiyo, Baadhi ya wakaazi mjini Marsabit wamewataka vijana wa Gen Zs kusitisha maadamano yao yaliyopangwa kufanyika hapo kesho na badala yake kumpa rais muda wa kufanya kazi haswa baada ya kutekeleza mageuzi kadhaa serekali. Baadhi ya waliozungumza idhaa hii wameyataja maadamao ya hapo kesho yaliyopewa jina NANENANE kama yanayolenga[Read More…]

WAFUGAJI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAHIMIZWA KUKUMBATIA KILIMO BIASHARA KAMA NJIA MOJA WAPO YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Na Grace Gumato, Wafugaji katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kukumbatia kilimo Biashara kama njia moja wapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Akizungumza na idhaa hii ofisi mwake afisa wa kilimo katika eneo bunge la Saku Dub Nura ametaja kuwa wafugaji wanafaa kuwa na mfumo mbadala ya kijikumu kimaisha[Read More…]

Subscribe to eNewsletter