IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Grace Gumato,
Wito umetolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi, zile za secondari na hata vyoo vikuu kutoshiriki katika wizi wa mitahani.
Akizungumza na idhaa hii Askofu wa kanisa la Kianglikani Askofu Qampicha Wario amesema kuwa wanafunzi wengi wamejitoza katika wizi wa mitihani na kupata alama za juu ambazo mwishowe huchangia mwanafunzi kushindwa kufanya kozi katika chuo kikuu na hata kufeli katika maisha.
Askofu Qampicha ameonya kuhusiana madhara yanayotoka na wizi wa mitihani akitaja mzazi kutumia pesa nyingi za karo na huchangia mwanafunzi kutojiamini katika maisha.
Hata hivyo Askofu Qampicha ameirai jamii kuwa kielelezo bora kwa watoto wao huku akisema kuwa ni vyema wazazi kuwafunza watoto wao maadili mema.