Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na Joseph Muchai Siku kadhaa baada ya mauaji ya watoto mapacha kuripotiwa katika eneo la Dukana eneobunge la North Horr imam wa msikiti wa jamia mjini Marsabit Sheikh Mohamed Noor amekemea kitendo hicho. Akiongea na kituo hiki Sheikh Noor amesema kuwa ni kinyume na haki za binadamu na pia sheria[Read More…]
Huku muhula wa kwanza katika kalenda ya masomo ukiendelea wafugaji jimboni Marsabit wamehimizwa kuwapeleka wanao shuleni. Ni himizo ambalo limetolewa na mhifadhi wa msitu wa Marsabit Mark Lenguro ambaye anasema kuwa baadhi ya wafugaji wanawanyima watoto haki yao ya kupata elimu kwa kuwapa majukumu nyumbani. Serikali imekuwa ikisisitiza haja ya[Read More…]
Shirika la hifadhi ya jamii la Melako limepinga Taarifa zilizopeperushwa na runinga moja ya kimataifa kuhusu utumizi mbaya ya fedha za hewa ya Carbon (Carbon credit funds), ambayo shirika hilo limekisiwa kutumia vibaya pamoja na madai mengine. Akizungumza na wanahabari kwa niaba ya Melako Community Conservancy, Joseph Lesoi amesema kuwa[Read More…]
Na Waandishi Wetu Mahakama ya Marsabit imeagiza kufukuliwa na kufanyiwa upasuaji, miili ya watoto mapacha waliouawa katika kijiji cha Dololo Boji kaunti ndogo ya Dukana katika kaunti ya Marsabit. Ni agizo ambalo limetolewa na hakimu mwandamizi wa mahakama ya Marsabit, Simon Arome ambaye ameagiza shughuli hiyo kufanyika katika muda wa[Read More…]
Wito umetolewa kwa wakaazi wa Marsabit kutembelea vituo mbalimbali vya watalii hapa jimboni ili kuimarisha uchumi wa jimbo. Kwa mujibu wa waziri wa jinsia na utalii katika kaunti ya Marsabit, Jeremiah Lendanyi, ni kuwa kaunti ya Marsabit ina vivutio vingi vya watalii na ambavyo vinaweza kuimarisha uchumi wa jimbo hili,[Read More…]
NA ISAAC WAIHENYA Idara ya jinsia kaunti ya Marsabit imelaani kisa cha mauaji ya watoto wawili mapacha waliouwawa katika eneo la Dololo kaunti ndogo ya North Horr. Kwa mujibu wa afisa mkuu katika idara ya jinsia Anna Marie Denge ni kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuona kwamba bado kuna jamii[Read More…]
NA CAROLINE WAFORO Idara ya misitu katika kaunti ya Marsabit sasa inasema kuwa imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa moto unaoshuhudiwa katika kaunti jirani ya Isiolo hauenei hadi katika jimbo hili la Marsabit. Akizungumza na shajara ya radio jangwani afisini mwake mhifadhi wa msitu wa Marsabit Mark Lenguro amesema kuwa idara[Read More…]
Na Samuel Kosgei Marehemu Padre Francisco Terragni ametajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia maskini na wasiojiweza kwa namna moja ama nyingine katika jamii. Padre mkuu wa parokia ya Dirib Gombo Fr George Guyo amesema kuwa marehemu Frank aliishi maisha ya chini na ya unyenyekevu bila kubagua hali ya mtu yeyote.[Read More…]
Jimbo katoliki la Marsabit linasikitika kutangaza kifo cha Padre Francisco (Frank) Terragni kilichotokea tarehe 17 Januari 2025 katika Hospitali ya Huruma kule Nanyuki Akidhibitisha taarifa hiyo Askofu wa Jimbo Katoliki la Marsabit Mhashamu Baba Askofu Peter Kihara amesema kwamba mwili wa marehemu utawasili na kupokelewa Marsabit hii leo tarehe 22 Januari[Read More…]
Shirikisho la soka nchini FKF tawi la Marsabit linaweka mikakati kambambe ya kuhakikisha kwamba maswala ya michezo yanaendelezwa kiutalamu na kwa mipangilio inayofaa. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa FKF tawi la Marsabit Godana Roba ni kuwa wanapanga kukutana kama washikadau mbalimbali katika sekta hiyo ili kulaini mambo pamoja na utendakazi[Read More…]