Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Baada ya waziri wa usalama wa ndani Profesa Kithure Kindiki kuteuliwa kama naibu wa rais mpya hii leo na Rais William Ruto, wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na uamuzi huo.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, wamemtaja Kindiki kama mtu anayefaa kushikilia wadhifa huo.
Pia wamemtaja Kindiki kama kiongozi atakayeunganisha Wakenya kinyume na alivyokuwa mtangulizi wake.
Aidha wengine wao wamehisi kuteuliuwa kwa Kindiki ni njama ya kuligawanya eneo la Mlima Kenya huku wakimtaka Kindiki kuwa makini na wadhifa huo.
Wametoa wito kwa Rais na Naibu wake mpya kushirikiana kwa pamoja ili waweze kuwafanyia Wakenya kazi.
Kuhusiana na swala la kung’olewa mamlakani kwa aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua baadhi ya wakaazi wametaja kusikitishwa na uamuzi uliotolewa na bunge la seneti hiyo jana jioni wa kumbadua ofisini wakihoji kwamba Gachagua hakupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Seneti.