HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Isaac Waihenya & Kame Wario,
Mashirika yanayoendeleza vita dhidi ya dhulma za kijinsia hapa jimboni Marsabit yanapania kuunda kamati maalum ya kuangazia namna ya kupunguza visa hivyo hapa jimboni.
Kwa mujibu wa afisa wa miradi katika shirika la MWADO Mary Nasibo, ni kuwa kamati hiyo itarahisisha mambo na kuhakikisha kwamba mbinu zinazotumika katika kupambana na visa vya dhulma za kijinsia zinafaulu.
Akizungumza wakati wa warsha iliyowaleta pamoja maafisa kutoka idara mbalimbali serekalini, maafiasa wa usalama pamoja na mashirika yasiyo-yakiserekali hapa jimboni, Nasibo amesema kuwa ukubwa wa kaunti na kukosekana kwa huduma za serekali karibu na wananchi hulemaza vita hivi kwa asilimia fulani.
Aidha Nasibo amesema kuwa mkao huo umelenga kuleta mawazo pamoja ili kutafuta mbinu mwafaka ya kukabiliana na kero la dhulma za kijinsia hapa jimboni Marsabit.
Hata hivyo Nasibo ametoa onyo kwa wale wanaoendeleza mila potovu kama vile ukeketaji na ndoa za mapema ambazo zinahujumu haki za watoto kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.