HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Isaac Waihenya,
Waadishi wa habari hapa jimboni Marsabit wametakiwa kufunguka kuhusiana na maswala yanayowadhiri ili kujizuia dhidi ya msongo wa mawazo.
Kwa mujibu wa mwanahabari Abraham Dale ambaye kwa sasa anafanaya kazi na shirika lisilo la kiserekali la MWADO ni kuwa muda mwingi wanahabari hukosa kuzungumza kuhusiana na yale wanapitia kazini na hata maishani mwao jambo linalohatarisha afya yao ya akili.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya simu Dale amewataka wanahabari pia kujipa breki muda mwingine ili kutuliza mawazo.
Aidha Dale ametoa wito kwa wasimamizi wa vituo vya habari wamiliki,mameneja na hata wahariri kuwapa muda wa kutosha wanahabari wa kushughulikia maswala yanayowadhiri kimaisha.
Dale amelitaja swala la ukosefu wa mishahara sawa na ugumu kazini kama sababu zinazochangia wanahabari kukumbwa na msongo wa mawazo.
Kauli ya Dale inajiri baada ya video ya aliyekuwa mwanahabari wa kituo cha NTV Nasibo Kabale kusambaa mitandaoni ikimwonyesha mwadada huyo akiwa anaishi mitaani baada ya kukumbwa na matatizo ya msongo wa mawazo.
Kwa sasa familia pamoja na marafiki wanachangisha pesa ili kuwahakikisha kwamba mwanahabari huyo anapata tiba.