IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Grace Gumato
Janga la ukame limetajwa kama mojawapo ya changamoto ambayo inachangia kina mama kutonyonyesha watoto wao katika kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii afisini mwake David Buke Halakhe afisa naye simamia lishe katika kaunti ya Marsabit amesema uwepo wa ukame umechangia akina mama wengi kukosa lishe bora na pia wengi wao kukosa chakula cha kutosha jambo linalochangia kupungua kwa hatua za kunyonyesha.
Aidha Buke ametoa wito kwa kina mama kuhakikisha kuwa wananyonyesha watoto miezi sita mfululizo kinyume na hulka ya kuwasitisha kunyonya mapema, ili kuwawezesha kuwa na afya njema.
Takwimu za idara ya afya ya mwaka iya 2022 zinaashiria kuwa ni asilimia 74.2 pekee ya wanawake wanaojifungua katika Kaunti ya Marsabit hunyonyesha watoto wao kwa muda wa chini ya saa moja akitaja kutohamasishwa kwa kina mama mashinani kuhusu umuhimu wa kunyonyesha kama sababu kuu.
Amesisitiza haja ya jamii kuhamasisha watoto wasichana wanaopata mimba za mapema umuhimu wa kunyonyesha mbali na kuwapa wanawake uhuru wa kunyonyesha watoto bila unyanyapaa wowote.