IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Caroline Waforo
Baada ya kisima cha Ririma kilichoko lokesheni ya Kargi eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit kuharibika na wakaazi kukosa maji kwa siku kadhaa msimamizi wa timu ya kurekebisha visima vya maji katika idara ya maji jimboni Marsabit Fakasa Boru Fakasa ametoa hakikisho la kukarabatiwa kwa kisima hicho kufikia jioni ya leo.
Fakasa aliyezungumza na shajara ya Radio Jangwani anasema kuwa tayari kuna timu inayoendeleza ukarabati wa kisima hicho.
Kulingana na Fakasa kunavyo visima zaidi vitakavyofanyiwa ukarabati ikiwemo kile cha Elebor katika kaunti ndogo ya Sololo na kile cha kambi nyoka kilichoko Diid Galgallo.
Na baada ya kisima cha Borri kilichoko eneo bunge la Moyale kusombwa na maji ya mafuriko karibu miezi minane iliyopita Fakasa anasema kuwa mikakati ipo ya kuchimba kisima kipya.