KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Isaac Waihenya,
Wito umetolewa kwa jamii ya Marsabit kutowatenga watu wanaoishi na matatizo ya afya ya akili.
Kwa mujibu wa mwazilishi wa shirika la Open Minds Community Focus (OMCF) linashughulikia maswala ya afya ya akili hapa jimboni Marsabit Bi. Mariam Abduba ni kuwa jamii imekuwa ikikosa kuwaelewa na hata kuwatelekeza watu wanaokubwa na matatizo ya afya ya akili jambo linalowadhiri zaidi.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Bi. Mariam ameitaja mila potovu kama mojawepo ya maswala ambayo yanapelekea vijana kukumbwa na matatizo ya afya ya akili.
Aidha Bi. Mariam amekariri kuwa tatitizo la afya ya akili pia limepekea ongezeko la idadi ya vijana wanaotumia mihadarati na dawa za kulevya swala analolitaja kwamba linafaa kuangaziwa haraka iwezekanavyo ili kuokoa kizazi kijacho.
Ameitaka jamii kuhakikisha kwamba inasaka msaada hitajika kwa wataalam wa afya na hata wataalam wa ushauri katika shirika la (OMCF) ili kuzuia madhara zaidi yanayotokana na ugongwa wa afya ya akili.