IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Isaac Waihenya,
Wito umetolewa kwa jamii ya Marsabit kukumbatia zoezi la upanzi wa miti ili kupambana na kero la mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la Inua Dada Mashinani, Jillo Fugicha ni kuwa kaunti ya Marsabit ndio imeadhirika mno kutoka na hali ya kiangazi ambayo inashuhudiwa hapa jimboni.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani Fugicha ametaja kwamba akinamama na wasichana ndio wanaadhirika zaidi ambapo baadhi ya jamii huwaoza watoto wao ili kuweza kujikimu kimaisha.
Aidha Fugicha amewarai washikadau mbalimbali kushirikiana ili kukabiliana na kero hilo.
Amekariri kuwa akinamama na watoto wameadhirika na ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia ambavyo vimetajwa kuongezeka maradufu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.