IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Grace Gumato
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wameonywa dhidi ya ununuzi wa dawa zozote bila kujua ugonjwa wanaogua ili kujiepusha na madhara kwenye miili yao.
Akizungumza na idhaa hii Amina Sharamo ambaye ni dakitari wa ngozi katika kaunti ya Marsabit ametaja kuwa watu wanaonunua dawa za ngozi bila kupata mwongozo kamili kutoka kwa daktari wako kwenye hatari ya kupata madhara katika nyuso zao.
Aidha sharamo amesema kuwa watu wengi wako na dhana Potovu kuhusiana na ugonjwa wa ngozi akitaja kuwa baadhi ya watu wanaogopa kutembelea kituo cha afya na kuishia kuenda kutumia dawa za kinyenji ambayo inawadhuru zaidi.
Hata hivyo sharamo wamewarai wakaazi wa Marsabit kutumia vipondozi ambavyo havitadhuru afya yao na pia amewahimiza wale ambao wako na shida ya ngozi kutembelea kituo cha afya ili kupata matibabu inayofaa.