IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na JB Nateleng,
Kufuatia makubaliano ya kurejea kazini kati ya chama cha walimu wa shule za upili na vyuo va kadri nchini (KUPPET) na tume ya kuwajiri walimu (TSC), walimu sasa wanatarajiwa kurejea shuleni kuendeleza kalenda ya masomo.
Akizungumza na wanahabari mjini Marsabit,katibu mtendaji wa KUPPET tawi la Marsabit Sarr Galgallo amesema kuwa muungano huo umeweza kuafikiana na TSC, kushughulikia matakwa yao huku akiwarai walimu kurejea shuleni.
Sarr ameusifia ushirikiano ulipo baina ya walimu wa shule za upili jimboni ambao walikuwa watulivu na wavumilivu hadi wakati ambapo makubaliano yakurejea kazini yalipofanyika akisema kuwa huo ni uzalendo ambayo muungano huo unajivunia.
Aidha Sarr amesema kuwa hakuna mwalimu ambaye anafaa kudhulumiwa kwa kukosa kuripoti shuleni wiki ya kwanza, na kuwataka walimu wote kuripoti visa vya dhulma kwa afisi ya KUPPET iliyopo karibu nao iwapo watadhulumiwa.
Hata hivyo mkuu huyo wa KUPPET jimboni Marsabit amewahimiza wazazi ambao waliwatoa wanawao shuleni kuwarejesha kwani sasa masomo yatarejelewa kama kawaida huku walimu wakipambana kuhakikisha kuwa wamefidia muda uliopotea.